UMAHIRI WA ASKARI POLISI WAMKOSHA NAIBU WAZIRI

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mheshimiwa Jumanne Sagini amekoshwa na umahiri wa askari Polisi waliopo mafunzo ya uongozi mdogo cheo cha sajini meja na Koplo walioonyesha wakati wa maonyesho mbalimbali ya kuhitimisha mafunzo ya medani za kivita Septemba 5, 2023 kambi ya kambapori iliyopo Kilimanjaro Magharibi.

Mhe. Sagini ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo hayo amesifu umahiri mkubwa wa askari hao katika kukabiliana na adui na ukakamavu mkubwa walioonyesha.

Sagini amesema kwa uwezo walionao askari hao ni wazi kwamba mafunzo yao yataleta tija katika kulinda wananchi na mali zao na kwamba jamii ya Watanzania ipo mikono salama kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.

Kwa upande mwingine Mhe. Sagini amewatunuku vyeti vya pongezi askari 10 waliofanya vizuri zaidi katika mafunzo hayo yaliyojumuisha askari 2212.

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa miezi mitatu yanatarajia kufungwa rasmi Septemba 6, 2023 katika viwanja vya kambi ya Polisi Kilelepori wilaya ya Siha na Mheshimiwa huyo kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ambaye yuko kwenye majukumu ya mkutano mkuu wa Jeshi hilo unaoendelea jijini Dar es salaam.

Dawati la habari Tps-Moshi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *