MH. SIMBACHAWENE AFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA TAKUKURU – MOSHI.

Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Mh. George Simbachawene leo tarehe 06.10.2023 katika Shule ya Polisi Tanzania- Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro amewafungia mafunzo Maofisa na maofisa wasaidizi mafunzo yao ya awali.

Hata hivyo, Mh. Simbachawene amewataka wahitimu kutumia taaluma waliyoipata kuifanya TAKUKURU kuwa ya mfano, kuheshimika na kuaminika katika jamii.

Pia amesema kuwa Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo hivyo ni jukumu la wahitimu hao na TAKUKURU kwa ujumla kuhakikisha zinatumika kikamilifu kulingana na malengo.

Aidha, amepongeza wakufunzi wote waliowezesha mafunzo hayo ya miezi mitano kufanyika kikamilifu.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini, Kamishina wa Polisi SALUM HAMDUNI amewataka wahitimu hao kwenda kufanya kazi kwa bidii na kuwataka wahitimu 23 ambao hawakufanya vizuri kwenye mitihani yao kubaki kwa muda wa mwezi mmoja ili kurudia masomo na mitihani yao. toka dawati la Habari TPS-Moshi

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *