Shule ya Polisi Tanzania Moshi yafaidika na URA SACCOS.

Leo Februari 26,2024, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) David Misime ambaye ni mjumbe wa Bodi ya URA SACCOS ameongoza makabidhiano ya Vifaa vya Matangazo ili kuongeza ubora wa uwasilishaji wa mihadhara kwa wanafunzi wanahudhuria na watakao hudhuria mafunzo mbalimbali katika Shule ya Polisi Tanzania.(TPS)
Akiongea na Mkuu na Wakufunzi wa shule hiyo,DCP Misime amesema hili limefanyika kwa ajili ya kurudisha fadhila kwa jamii kwa mujibu wa msingi wa saba wa Vyama vya Ushirika .
URA SACCOS baada ya kuona uhitaji wa Shule ya Polisi Tanzania ikaona itimize msingi huo wa saba kwa kununua vifaa hivyo vya matangazo ili wanafunzi waweze kufundishwa kwa kutumia ili kuweza kusikia vizuri na kuelewa ili wakahudumie watanzania katika viwango vinavyotakiwa kutokana na weledi watakao upata.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ramadhani Mungi ambaye ndiye Mkuu wa wa Shule ya Polisi Tanzania, ametoa shukrani za dhati kwa Mlezi wa URA SACCOS,Mkuu wa Jeshi la Polisi Cammilus Wambura IGP, na Uongozi mzima wa URA SACCOS kwa kukilea chama vizuri na hatimae kuweza kurudisha shukrani kwa Jamii.
SACP Mungi alimalizia kwa kuahidi kuvitunza vifaa hivyo na kwamba vitafanya kazi iliyokusudiwa.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *