Leo 02/03/2024 Wakuu wa Kombania zote za Shule ya Polisi Tanzania Moshi wamefanya Vikao na wanafunzi wa kombania ,Ambapo Asp PAZZIA M.STEPHEN ni OC wa Kombania A Ambaye ana jumla ya wanafunzi 971 ,Asp Athumani H. lovissinga OC Kombania Kuu , Asp Nassoro A. Mkwama OC Kombania B akiwa na wanafunzi 968 na Asp Ngonji C. Stambuli Kaimu OC Kombania C ,ambaye ana wanafunzi 962
Lengo la Vikao hivi ni Kuwakumbusha kuwa Wazalendo na Nchi yao lakini pia kwa Jeshi na Shule kwa ujumla,kuwakaribisha ,kuufahamu uongozi wa kombania walimu na kuwapa maelekezo kuhusiana na mafunzo nidhamu, usafi, sheria za shule.
pia kutokujihusisha na mambo mabaya yenye kusababisha kufukuzwa mafunzo kuwaheshimu wakufunzi kuwa na nidhamu na hata baada ya kumaliza Mafunzo
Katika kuhitimisha vikao hivi Wanafunzi Wamekumbushwa na kuelezwa kwa nini wako hapa shuleni na kuwambusha Dira na dhima ya shule yao ,vithaminiwa vya Shule na utamaduni wa kipolisi .
Serikali yetu inafanya vizuri sana
Nikiwa kama mzarendo, nawezaje kupata taarifa za nafasi za kujiunga na chuo hiki?