NBC NA EXIM ZATOA MSAADA WA VITANDA TPS -MOSHI
Benki za NBC pamoja na EXIM leo tarehe 24.04.2024 zimetoa msaada wa jumla ya vitanda 68 kwa shule ya Polisi Tanzania – Moshi.Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa makabidhiano ya vitanda hivyo Commandant wa shule hiyo, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi RAMADHANI MUNGI amezishukuru benki hizo na kuziomba kuendeleza mshikamano huo.Aidha, LAZARO MOLLEL, meneja wa NBC – Moshi pamoja na STANLEY KAFU, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano EXIM wameahidi kuendeleza ushirikiano kwani Jeshi la Polisi nchini limekuwa taasisi muhimu sana kuhakikisha usalama wa mali za Benki hizo.