GWARIDE
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura akikagua gwaride wakati wa hafla ya kuwavisha Nishani maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla iliyofanyika Shule ya Polisi Moshi Mkoani Kilimanjaro Mei 22,2024.
Nishani hizo walipewa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.