NISHANI
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura akimvalisha Nishani ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi Mkoani Kilimanjaro SACP Ramadhani Mungi na wengine kwaniaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla iliyofanyika Shule ya Polisi Moshi Mkoani Kilimanjaro Mei 22,2024.
Nishani hizo walipewa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.