TPS WACHANGIA DAMU SALAMA
Leo tarehe 31.05.2024, wakufunzi na wanafunzi wa Shule ya Polisi – Moshi, wamechangia damu salama kwa hospitali za KCMC pamoja na Mawenzi.
Akiongoza zoezi hilo kwa niaba ya Commandant wa shule ya Polisi Tanzania – Moshi, Mnadhimu wa shule hiyo Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi STANLEY KULYAMO, amesema ushirikiano mzuri uliopo kwa Jeshi la Polisi ndio unapelekea msukumo wa kujitoa kwao.
Naye, VICTORIA BANDIHAI, mratibu wa damu salama Mkoa wa Kilimanjaro ametoa shukurani kwa Shule ya Polisi Tanzania -Moshi kwa mchango wa damu hiyo utasaidia kuokoa maisha.