SERIKALI KUONGEZA AJIRA JESHI LA POLISI NCHINI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. ALLY SENGA GUGU amesema Serikali ina mpango wa kuongeza uandikishaji wa askari wapya kwa Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama nchini.Amesema hayo leo tarehe 28.06.2024 huko Kambi ya Kilele Pori iliyopo wilayani Siha, Mkoani Kilimanjaro wakati akifunga mafunzo ya uongozi mdogo ngazi ya Koplo kozi iliyoendeshwa na Shule ya Polisi Tanzania – Moshi.Mh. GUGU amewataka Wahitimu wote kuwa na nidhamu na kusimamia askari wa chini yao kutenda kazi kwa weledi.Aidha, amewataka kutambua dhamana lililopewa Jeshi la Polisi katika kulinda na kusimamia usalama nchini na kuwataka kujiepusha na vitendo vya rushwa pamoja na biashara haramu ya dawa za kulevya. Naye Naibu Kamishna wa Polisi ANTHONY RUTASHUBURUGUKWA amewataka wahitimu wote kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia misingi yote kama walivyofundishwa na kujiendeleza kwa kupata mafunzo mbalimbali ili kuongeza ujuzi na maarifa yatakayoboresha utendaji ndani ya Jeshi la Polisi nchini

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *