WANAFUNZI WA MAFUNZO YA UONGOZI MDOGO NDANI YA JESHI LA POLISI NGAZI YA CPL WALIOPO KAMBI YA KILELEPORI WAFANYA USAFI KATIKA ZAHANATI YA SINAI

Leo tarehe 26/12/2024 kuanzia saa 02:00 Hadi 06:00 Asubuhi siku ya mapumziko ya Christmas wanafunzi 200 wa mafunzo ya uongozi mdogo ndani ya jeshi la Polisi ngazi ya CPL waliopo kambi ya Kilelepori wakiongozwa na Adjutant wa shule ya Polisi Tanzania – Moshi SSP A.S. Damazo, wakaguzi wasaidizi 02; A/INSP Ramadhani na A/INSP Machaule na G.3179 SGT Othman PRO Kilelepori wamefanya usafi katika zahanati ya Kijiji Cha Sinai KM 05 kutoka Kambini, katika Kijiji Cha Sinai,kata ya Ormelili,Tarafa ya Siha kusini, wilaya ya Siha, mkoa wa Kilimanjaro.
Aidha, diwani wa kata ya Ormelili ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Siha Mh Noel Philimon Mollel, mtendaji wa kijiji cha Sinai Mh Mohamed Ally Zuberi, Mganga mfawidhi wa zahanati ya Sinai Dr.Johanitha Kabyazi Sylvester na viongozi wengine wa kata na Kijiji wamelishukuru jeshi la Polisi kwa zoezi hili na kuahidi kuendelea kushirikiana na jeshi la Polisi katika shughuli mbalimbali.
Zoezi hili ni mwendelezo wa shughuli zinazofanywa na Shule yetu ili kuwa karibu na jamii inayotuzunguka na ni jitihada za Jeshi la Polisi Tanzania kushirikiana na jamii katika shughuli mbalimbali za kijamii Ili kuweza kubaini na kuzuia uhalifu katika maeneo yao.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *