March 20, 2025
•
2 min read
Afisa Mnadhimu Utawala SACP Stanley Kabiki Kulyamo ambaye pia ni Kaimu Commandant wa Shule ya Polisi Tanzania Moshi amefungua rasmi mafunzo ya Uongozi Mdogo Jeshini ngazi ya cheo cha Sajini (Sergeant) leo tarehe 19/03/2025 ikiwa ni kozi no.2/2024/2025.Aidha kabla ya ufunguzi huo,Kaimu commandant Sacp Stanley Kulyamo Ameanza kwa kumshukuru sana Mhe.Dr.Samia Suluhu Hassan-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kwa kuendelea kuliboresha Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na kutoa vyeo vingi kupitia kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Afande Camillus M.Wambura,kisha aliwakaribisha shuleni na kuwataka wajitambue kwa kiasi kikubwa kwani Jeshi la Polisi na Taifa zima wana imani kubwa na kada hiyo ya Sajini, tena aliwataka kuzingatia kilichowaleta ambacho ni Mafunzo huku wakiwa na maadili mema hatimaye kuimarika kwa suala zima la nidhamu ya mtu mmoja kisha Jeshi kwa ujumla.Akiongea na wanafunzi amewataka kuheshimu na kufuata sheria za shule na kutokufanya kosa lolote vinginevyo hakutakuwa na maana yoyote ya kuwaongezea majukumu wakati hayo ya CPL yamewashinda.Hivyo alitoa wito kwa Wakufunzi kuwasimamia kwa kuzingatia Amri zinazowamiliki Wanafunzi wawapo mafunzoni na kwa yeyote atakayekwenda kinyume na taratibu za shule au za Jeshi ataachishwa Mafunzo au kufukuzwa kazi mara moja. SACP Kulyamo Ameendelea kuwakumbusha kuwa mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa kuchagua viongozi na si bora viongozi na kwa sisi Watumishi suala la uchaguzi,mbali na kwamba ni haki yetu kikatiba lakini ni muhimu sana kwetu kwani "mwenye macho haambiwi ona". Tena,aliwakumbusha kuwa kila mmoja wao lazima aboresha taarifa zake katika Daftari la Mpiga Kura ili kuitendea haki ya kikatiba hivyo ni lazima kila mmoja kuwa na kitambulisho cha mpiga kura.Kisha alirudia kuwataka kizingatia mafunzo ikiwa ni pamoja na kuzingatia wajibu mzima wa mpiga kura na majukumu mazima ya Jeshi la Polisi. Mwisho,amerudia kumshukuru Mhe.Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliboresha Jeshi na kuendelea kupandisha vyeo Askari kwa ngazi mbalimbali pamoja na kuboresha miundombinu ndani ya Jeshi la Polisi.