Explore exciting opportunities from Tanzania Police innovation.
Tps Moshi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, leo tarehe 11 Agosti 2025, amefungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi ambapo ufunguzi uo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Polisi Tanzania Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Tps Moshi
Katika ziara hiyo alipokelewa na Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania Moshi (TPS-Moshi), SACP Ramadhani A. Mungi pamoja na Mafisa wengine
Tps Moshi
Kamishna wa Polisi Jamii, CP Faustine Shilogile leo Julai 31, 2025 amefungua mkutano mkuu wa mwaka wa mfuko wa faraja wa Jeshi la Polisi kwa kupongeza kuanzishwa kwa mfumo unaoendesha na kuratibu utoaji huduma za mfuko huo ambao hadi sasa umesajili asiliamia 60 ya watumishi wote wa Jeshi la Polisi katika mfumo wa kidijitali.Kamishna Shilogile amewasisitiza viongozi wa mfuko huo kutoa elimu kwa wajumbe kuhusu utolewaji wa huduma kwa njia ya Kidigitali na kutoa mrejesho wa huduma zilizotolewa kwa wanachama na kuhakikisha kuwa mfuko unatoa huduma kusudiwa kwa walengwa kwa ufasaha na kwa wakati ili lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo liweze kutimizwa ipasavyo.
Tps Moshi
Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imetoa mafunzo ya kusimamia usalama wa mifumo ya TEHAMA serikalini kwa Maafisa, Wakaguzi na Askari wa ngazi ya kawaida katika Shule ya Polisi Tanzania Moshi (TPS) Ambapo lengo la mafunzo hayo ni kulinda na kutuma taarifa muhimu, kukinga taarifa zisitumike bila idhini, kulinda taswira na kupima uhimilivu wa mifumo pamoja na kupendekeza teknolojia sahihi pasipo na gharama kwa taasisi.