KAMISHNA SHILOGILE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA MFUKO WA FARAJA WA JESHI LA POLISI

November 8, 2025 · Tps Moshi • 1 min read
Kamishna wa Polisi Jamii, CP Faustine Shilogile leo Julai 31, 2025 amefungua mkutano mkuu wa mwaka wa mfuko wa faraja wa Jeshi la Polisi kwa kupongeza kuanzishwa kwa mfumo unaoendesha na kuratibu utoaji huduma za mfuko huo ambao hadi sasa umesajili asiliamia 60 ya watumishi wote wa Jeshi la Polisi katika mfumo wa kidijitali.Kamishna Shilogile amewasisitiza viongozi wa mfuko huo kutoa elimu kwa wajumbe kuhusu utolewaji wa huduma kwa njia ya Kidigitali na kutoa mrejesho wa huduma zilizotolewa kwa wanachama na kuhakikisha kuwa mfuko unatoa huduma kusudiwa kwa walengwa kwa ufasaha na kwa wakati ili lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo liweze kutimizwa ipasavyo.