ACP KISALO AONGOZA ROUTE MARCH

June 5, 2026 1 min read
Leo tarehe 06/06/2026, Mkufunzi Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania Moshi na Kaimu Mkuu wa Utawala, ACP Omary Kisalo, ameongoza zoezi la Route March lililowashirikisha wakufunzi wote wa Shule ya Polisi Tanzania Moshi. Akizungumza baada ya zoezi hilo, ACP Kisalo amewataka wakufunzi kuendelea kushiriki mazoezi mbalimbali ya viungo ili kuimarisha afya za miili yao na kujikinga dhidi ya magonjwa nyemelezi. Aidha, amesema kuwa mazoezi hayo yatakuwa endelevu na yatafanyika kila Jumamosi, huku akiwahimiza wakufunzi wote kushiriki kikamilifu.