June 5, 2026
•
1 min read
Leo, tarehe 05/06/2026 Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Ramadhan Kingai amefunga kikao kazi cha kuwajengea uwezo washiriki 215 wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai kutoka mikoa, wilaya na vikosi mbalimbali nchini.Ambapo mafunzo hayo yamefanyika katika Sule ya Polisi Tanzania Moshi Katika hotuba yake, aliwashukuru washiriki kwa ushiriki wao mzuri na kuwataka kutumia maarifa waliyopata kuongeza weledi, uadilifu na ufanisi katika uchunguzi wa kisayansi ili kuhakikisha haki inatendeka. Aidha, alisisitiza umuhimu wa matumizi ya sayansi na teknolojia katika kukabiliana na uhalifu wa kisasa pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai na Kamisheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai. Mwisho, aliwataka washiriki kuwa mabalozi wa maarifa hayo katika maeneo yao ya kazi kabla ya kutangaza rasmi kufungwa kwa kikao kazi hicho.