August 12, 2025
•
1 min read
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amesema Jeshi hilo halitawavumilia watu wanaojificha chini ya mwamvuli wa siasa ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kufanya vitendo vya uhalifu wakiwa na dhamira ya kuvuruga amani ya nchi. Amesema watu hao wamekuwa wakitumia lugha za uchochezi na upotoshaji kwa lengo la kuigawa jamii, na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria.