WASTAAFU WATAKIWA KUWA KIELELEZO

August 21, 2026 • 1 min read
WASTAAFU WATAKIWA KUWA KIELELEZO

Mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, GODFREY MZAVA, amewataka wastaafu wa Jeshi la Polisi kuwa kielelezo chema katika maisha yao baada ya kustaafu utumishi wa umma.

Akizungumza tarehe 21/08/2026 wakati wa hafla ya kuwaaga askari 22 waliostaafu kazi ya utumishi wa umma waliokuwa wakifanya kazi kituo cha Shule ya Polisi Tanzania - Moshi, amesema wastaafu wanapaswa kuwa kielelezo cha maisha mema.

Aidha, amewataka kuendelea kuishi viapo vyao, huku wakitumia fursa zilizopo huko waendako kujiimarisha kiuchumi, pia wakiendelea kutunza afya zao.

Naye Komandanti wa shule hiyo, SACP Ramadhani A. Mungi, amewapongeza wastaafu hao, ambapo amesema mchango wao katika taifa la Tanzania utakumbukwa daima.